Ni hadithi ya kutisha inayohusu safari ya binti kwa jina la Alice katika kupigani maisha ya mpenzi wake Kelvin dhidi ya v majini na viumbe vya kutisha ,katika safari hiyo ianakutana na mambo mengi ya ajavu ikiwa kutenganishwa na familia yake
na kuishi katika dunia ambayo siyo yake
….usikose kufuatilia kisa hiki
UTANGULIZI
Katikati ya bahari moja iliyojulikana kwa jina la BAHARI YA HOPE iliyokuwa karibu na kijiji kimoja kilichojulikana kama KIJIJI CHA KASONGO , palikuwepo siri kubwa iliyokuwa imefichwa, siri ya ulimwengu wa majini, ambao binadamu walikuwa hawawezi kuufikia. Katika ulimwengu huo wa ajabu , alikuwapo , binti mrembo ambaye hakuwa binadamu wa kawaida alikuwa ni samaki mtu ambao wengi hupenda kuwaita NGUVA .jina lake aliitwa Alice Urembo wake haukufananishwa na kitu chochote katika dunia hii, na macho
yake yalikuwa mazuri mithili ya nyota
zing’aazo angani wakati wa usiku. Lakini licha ya uzuri wake, Alice alikuwa na kiu moja – kiu ya kupenda na kupendwa kwa dhati, kitu ambacho hakikuweza kupatikana katika ulimwengu wa bahari.
Upande mwingine wa hadithi, kulikuwa na Kelvin, kijana wa kawaida mwenye ndoto kubwa lakini maisha yake yalikuwa yamejaa changamoto. Hakuwahi kufikiria kwamba hatima yake ingeunganishwa na kiumbe wa ajabu kutoka baharini.
Lakini je, mapenzi kati ya binadamu na nguvu yanaweza kuvuka vikwazo vya dunia
na bahari? Je, nguvu ya upendo inaweza
kushinda hofu, tamaa, na chuki zinazotoka kwa pande zote mbili?
“Binti Nguvu” ni hadithi ya kusisimua ya mapenzi, usaliti, na ujasiri wa kupigania kinachozidi mipaka ya kawaida. Hii ni hadithi ya ulimwengu wawili tofauti, lakini moyo mmoja. Hii ni hadithi ya Alice na Kelvin.
hadithi inaanza ikiwa ni majira ya usiku, katika nyumba moja ambayo ilikuwa sio mbali sana na bahari. Kuna kijana mmoja kwa jina la kelvin alishtuka kutoka usingizini baada ya kuhisi kuna kitu kimeanguka kutoka juu ya bati. Alifungua mlango cha ajabu hakuweza kuona kitu . kijana huyu anajihusisha na uvuvi na hakuna mvuvi ambaye alikuwa akikubalika kumzidi kelvin na kila mtu alikuwa anajivunia sana shughuli yake ya uvuvi kwa sababu ilikuwa inamuingizia sana pesa na alikuwa akiitumia kuwasaidia na kuwatumia wazazi wake waliopo mkoani mwanza na wote walimtegemea yeye sio
hao tu hata ndugu walikuwa
wakimtegemea sana kelvin.
Licha ya yote hayo ,hata mabinti waliamini kama wakipata nafasi kwa kelvin watapata maokoto(pesa ) hivyo kila mtu alijaribu bahati yake lakini wapi kelvin alikuwa akiwakataa na kuwambia “huu sio muda wa kupenda ni muda wa kutafuta hela kipindi nmevubaa mlikuwa mnanikataa lakini kwa sasa ….. siwezi kudate na mtu yoyote ” . Wasichana walimchukia sana na kusema “hili kaka lina linga na vihela vyake ,mara oooooh akipata mwanamke ata mvubaza “.
lakini kama wahenga wasemavyo kelele za
chura hazimzuii tembo kunywa maji” . Basi tuendelee jina la kelvin lilivuma sana katika bahari hiyo iliyojulikana kwa jina la HOPE.
BAHARI YA HOPE ilipewa jina hilo kutokana na jinsi lilivyokuwa linavutia sana na aina ya samaki waliopo baharini ndo maana waliipa HOPE ikiwa na maana matumaini na wengi walitumia maeneo ya kando ya bahari kutuliza mambo mbali mbali ikiwa ni msongo wa mawazo ,na kila kitu na iliaminika kila aliyeenda pale na matatizo yake huisha.
Lakini pia kutokana na umaarufu na uhodari wa kelvin wavuvi wengi
walimchukia sana kwa kuona anafanikiwa
zaidi yao . Lakini kelvin alipambana na hiyo hali na ndio maisha ndugu zangu wasomaji ukitaka kufanikiwa usiogope maneno ya watu kwa sababu mwanadamu amepewa mdomo hivyo huwezi kumzuia kuzungumza wewe mtegemee MUNGU tu, kwa sababu hao wanaokusema vibaya vinywa wamepewa na huyo umuombaye na kumtegemea tuendelee sasa …………….
Basi alitoka njee kutazama nini hicho kimeanguka ???? lakini cha ajabu hakuweza kuona chochote akajisemea tena huku akicheka “hahaha… mawenge aya sijuwi nilikuwa nawaza nini mimi ila
sio mbaya ngoja nifanye fanye hesabu
maana leo nimeuza sana samaki na nilipata hela nyingi ngoja nizihesabu ili kesho niende mjini nikaziweke benki ….
Alianza kuhesabu hela zake alihesabu hela kwa muda mrefu sana na hela zilikuwa nyingi sana . mara rafiki yake kipenzi aliyeitwa Goodluck alimpigia simu
. simu iliita wimbo mmoja ambao uliimbwa na msanii aliyeitwa Goodluck Gozbet wimbo huo unaitwa unanipenda kama huujuwi unaweza ukaudownload uusikilize ni mzuri uliimba ivi kabla hajapokea………..
” na nimeamini nikitazama ,
nyuma ni kweli ulinipenda ,
na sikuwa hivi, ila ni wako wema, ni kweli ulinipenda “
kisha kelvin alipokea simu haraka sana na kusema ” namu Goodluck, habari yako “
“aiseeee salama ndugu yangu za huko” alisema Goodluck kwa sauti ya kujiamini.
“kwangu ni salama kaka ,vipi kaka mbona simu usiku , ndugu yangu kuna shida ?? aliuliza kelvin
“ndiyo mwanangu anaumwa sana na sina hela hapo nipo hospitali nadaiwa kama 50000 hivi sijuwi ata natoa wapi !!!!?
” usijali nakutumia sasa ivi si kwenye namba hiii” aliuliza kelvin
“ndiyo kaka nashukuru sana mungu
akulinde rafiki yangu ” alisema Goodkuck akionyesha shukrani kubwa sana ……
“usijali sisi ni ndugu lazima tushirikiane “. Basi maongezi yao yaliisha na baada ya dakika kadhaaa kwenye simu ya Goodluck muamala uliingia imethibitishwa
……………
Goodluck alishukuru maana mtoto wake alikuwa anaumwa sana.
Basi kelvin alihesabu pesa kisha akasema hizi kesho ntaziweka benki na baada ya hapo nitaendelea na mambo mengine , mara ghafla akahisi kama.kuna kitu tena
nje kimepita kama upepo
vuuuuuuuuuuuuuuuuuh …….
Alisita kidogo lakini alimua kuficha hela
.kisha kutoka nje akamuona mwanamke kavaa gaunl refu jeusi huku gauni lake likiburuzika chini .
Alikuwa akitembea kana kwamba anamtaka kelvin amfuate nyuma na kitu cha ajabu kelvin alimfuata kwa nyuma alizidi kutembea huku akiona tu mgongo wa binti na si sura yake alitembea umbali mrefu sana . lakini alipofika mbele aliangaza kila sehemu hakuweza kuona mtu yoyote yule zaidi zaidi upepo tu ukipiga taratibu sio siri aliogopa sana na kujiuliza kwa sauti ndogo”yule binti
nilikuwa namfuata sio muda hapa kaenda
wapi huyu , na angalia sehemu ilivikuwa kubwa na sio rahisi kwa binadamu kutembea haraka hivi ” lakini aligeuka nyuma kwa mbali aliona nyumba yake ikiwaka moto
ooooooh kichwani mwake lilikuja wazo zito “hela” alichomoka kama mshale
,mbio mbio kukimbilia hela zake alikimbia huku anahema sana yaani kana kwamba anakimbizwa na simba na baada ya muda mfupi alikuta hela nyumba yake yote imeungua duuuuh lilikuwa ni pigo kubwa sana alilia kama mtoto …
“yaaani mimi kupapambana kote ,leo malipo ni haya . nani kachoma numba
yangu? na kwanini kaichoma ? sijawahi
gombana na mtu hata kupigizana nao kelele??. kwanini leo wanilipe hivi ???
lakini alihisi kitu na kusema “hebu ngoja kwa hiyo huyu binti alitumwa anizuge yaani anizubaishe ili nyuma yangu wachome mote sio?? lakini je wangechoma nikiwa ndani si ningekufa mimi ? hivyo sielewi binti kanisaidia au yupo kwenye mpango huo wa kuchoma nyumba yangu. Watu wa karibu walifika na kujaribu kuzima lakini haikusaidia kitu
….
Goodluck kwa upande wa pili anapokea simu lakini alisogea pembeni kidogo ili
mkewe asisikie maongezi ghafla sauti
ilisikika
“tumeshachoma nyumba ya kelvin kama ulivotuagiza bosi na yeye amefia humo humo ndani” daaah kweli kikulacho ki nguoni mwako kumbe Goodluck ndo kafanya hila hizo …….
Goodluck alikata simu na kusema ” hahhaah bora ufe haiwezekani mimi nisome mpaka chuo hafu wewe unizidi hela na ukizingatia umeishia kidato cha nne bora umekufa na mtoto wala haumwi nilitaka kujua kama upo nyumbani ” duuuuuuh muda huo kelvin anajua ana rafiki kumbe ni adui
INAENDELEA
0 Comments