Basi tunaendelea pale pale tulipoishia baada ya kuona kuwa ashakamilisha lengo lake Goodluck alifurahi na kuamua kurejea kurudi kitandani aendelee kulala . lakini bila kujua alichokifanya kimempa maumivu gani rafiki yake ambaye hajaugundua unafiki wake …
UPANDE WA KELVIN
Alibaki ametahamaki pale hana la kufanya hela zenyewe ndo kapoteza sio hela tu kuanzia simu na kila kitu alikipoteza kwa sasa hana jipya mjini waswahili husema
hana chake kimemlamba mmmh
inasikitisha sana lakini alijisemea moyoni mwake ” ridhiki autoye ni Mungu na aitwaaye ni yeye mwenyewe hivyo sitakiwi kulala mika sana ,maana kama imeandikwa nitapata nitapata tu” huku anajipiga piga kifuani .
Mara ghafla mvua ikaanza kunyesha ohoooooo mbaya hiyo kwa kelvin alijaribu kukata majani ya minazi ajistiri lakini wapi radi zilipida sana ikabidi akimbilie kwa rafiki yake
ambaye hawakuwa na ukaribu sana zaidi ya salamu na ilikuwa ni majira ya usiku sana …
Alipofika kwa huyo jirani yake alimgongea
mlango mara tatu ngo! ngo! ngo! yule jirani aliitika kwa sauti nakuja alipofika pale aliufungua mlango na kumkuta kelvin akiwa kanyeshewa na mvua . Alimsikitikia na kumwambia pole sana ndugu kwa yaliyokukuta lakini jaah ni mwema atakuepuehia
Kelvin alijibu “oooooh nashukuru sana maneno yako yananipa nguvu ya kuendelea sasa ndugu yangu naomba nipate hata kahifadhi hata hapa eneo la jiko japo nijistili na haka kamvua sina kwa kwenda zaidi ya kuja hapa kwako kaka……
“daaah najua rafiki yangu huna hadhi ya kulala jikoni lakini unajua nina chumba
kimoja tu na unajuwa mimi , mke wagu na
kichanga chetu ndo kwanza tunajitafuta tafuta hivyo naomba ujikaze tu kwa leo nipo tayari kesho kukupangia chumba ata kwa mwezi mmoja tu rafiki yangu”
hata usjali sana we nisaidie tu nilale hapa kwa leo tu … alijibu kelvin
Emanuel alimpa kelvin blanketi kisha kumuonyesha jiko ili aweze kulala basi baada ya muda wa nusu saa kelvim alipitiwa na usingizi na ikamjia ndoto yq kumstajabisha kidogo ……..
Alikuwa yupo katika shughuli zake za uvuvi alikuwa ndani ya Bahari ya hope akitumia mtumbwi wake mara ghafla hali ya hewa ikabadilika na upepo ukawa mkali kiasi kwamba alipoteza control na kuingia
ndani ya maji ,alikuwa mtalamu sana wa
kuogelea aliogelea cha ajabu akiwa chini ya maji aliona kama geti hivi ilimpasa apite naye baada ya kupita hivi geti lilijifunga akashangaa ametokea sehemu nyingine ambayo ilikuwa ina fanana sana na ya dunia ya kawaida
“Hapa ni wapi tena mbona kama tumeanza kutishana “
Alipotazama mbele aliona kasiri moja kubwa sana napo zungumzia kasiri nazungumzia jumba moja kubwa sana. Alijiuliza nani anaishi pale lakini alikosa majibu alisogea hadi sehemu palipokuwa na geti alilikuta liko wazi …..
Alipotaka kupiga hatua kuingia ndani sauti ya mwanamke ilisikika “usiiiingie humo
ndani utakufa fanya vyote lakini usiingie
humo ..”
Lakini sauti ya pili “Kijana ingia huku ndo kuna sulurisho na ni njia pekee ya kurudi kwenu
Yule binti alimuasa sana lakini wapi alifungua mlango na kuingia alikutana na joka kubwa sana limetanua mdomo tayari kummeza
Hapo alishtuka kutoka usingizini na kujikuta amelala ufweni ilihali ule muda alilala mule jikoni kugeuka alikuta kundi la watu wengi kwenye nyumba ya Emanuel
“kheee imekuaje tene ,kwanza nimefikaje
hapa icho ndo natakiwa kujua ???? na cha pili nini kinaendelea pale ????.
Alisogea mpaka kwenye umati wa watu huwezi amini alikuta Emanuel mkewe na mtoto wake mtoto wake wote wamechomwa Chomwa visu …..
Alijisemea moyoni mwake “nini kinaendelea mpaka mtu ananinyanyua na kunitoa jikoni na kunilaza ufukweni ina maana nina usingizi kiasi gani???
Watu walikuwa wanaongea ongea maneno mengi sana ambayo kwa kelvin yalikuwa yanamuumiza sana sio siri
maana Emanuel alikuwa rafiki yake na
mtu aliyempa msaada …
Alirudi ufukweni akiwa na huzuni na wasiwasi haukupita muda baada ya kukaa pale ufukweni alikuja binti mmoja mrembo sana ana nywele ndefu macho ya kusinzia, ngozi yake lain na nyeupe sio siri alikuwa ni mrembo si kwenye macho ya kelvi tu ata kwa watu wengine ……
Alimsogelea kelvin na kukaaa karibu yake alikuwa katabasamu
“mambo kelvin vipi hali yako kaka” alisema alice akiwa katabasamu
“si salama si unaona huu msiba hapa ni rafiki yangu kipenzi na jirani yangu ,hata
jana tu na mimi nyumba yangu ilichomwa
moto “alisema kelvin kwa sauti ya masikitiko
“pole sana kanambia mama mmoja juu ya yale yaliyokukuta hakika umepitia mengi kaka lakini naamini utashinda zaidi na zaidi cha msingi jipe moyo. Naumwamini mungu …”
Asante sana dada kwa maneno yako hakika yamenipa faraja kubwa sana samahani sikukuuliza j ata jina na sehemu unayoishi ???? aliuliza kelvin
“oooooh naitwa Alice ni mgeni maeneo
haya hata nikikuelekeza huwezi kupajua ila sio mbali sana na hapa !!!!! alijibu alice
Lakini wakiwa wamekaa pale wanaongea mara ghafla mvua ikaanza kunyesha mmmmmh Alice alipatwa na wasiwasi mwili ulipanda joto akawa anatetemeka sana na jasho zipo zinatirrrika tu . Mkono wake wa kushoto ukaanza kutoa magamba enheeeee….nini kitaendelea
0 Comments