Basi tunaendelea pale pale tulipoishia baada ya Alice kuota magamba ya
samaki. ndipo tunapogundua kuwa yule
binti sio kiumbe wa kawaida . Akawa anamwambia kelvin kwa hasira “yatupasa tuondoke hapa kelvin” muda mwili wake ushaanzq kusisismuka mara ghafa kuna kundi la watu walikuwa wanapita mbio mbio hivyo walikuwa wanawapush na kwakuwa msongamano ulikuwa mkubwa sana ….
Baada ya dakika mbili msongamano uloisha lakini kelvin kuja kuangalia vizuri hakuweza kumuona mtu yoyote yule akasema “kheee ina maana huyu Alice kaenda wapi maaana ni ghafla “. Lakini aliona asijali kuhusu hilo suala maana binti alikutana naye pale pale hivyo hata kama kaondoka yeye haimuhusu ….
Alikimbia mpaka upenuni mwa nyumba
moja hivi iliyokaribu sana na eneo hilo maana mvua ilikuwa kubwa na hakuna kwa kwenda ….
Lakini ukisikia siku ambayo ameyakanyags ni leo unajua kwanini ?? kwa sababu mmoja ya mabinti ambaye aliwahi kuwakataa aliishi pale na kwa bahati mbaya binti alimuona akasema “leo nitakuonesha mpumbavu wewe”
duuuuh akachukua maukoko ya ugali na kuyakwangua vizuri huku akisema hakika leo kelvin kayakanyaga yaani alinikata mimi mbona shape ninayo mwendo upo sura nawachanganya wanaume wote hili
eneo yeye anikatae kweli daaah leo
nitamuonyesha
akatoka na yale makoko akijifanya kama hajaona hivi ikasikika ndani haloooooooooooo
Pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah usoni mwa kelvin kelvin alijifuta na kusema
“nipo hapa jamani najistiri na mvua hiii”
Binti huyo anaitwa tina alijibu yaani kana kwamba ni bahati mbaya “ooooooh sijuwi aiseee sikukuona mara oooih pole jamani mkaka handsome” lakini moyoni mwake
“kelvin wa kunikataa mm kweli sasa huu msimu akiinuka mshale akiinama mshale yaani mpaka aseme mi na kasoro gani
,maana sijawahi kukataliwa na
mwanaume mimi ndo huwa nawakataa kwa nini yeye???
Kelvin alijifuta na akiwa na furaha kidogo”usijali kuhusu hili ni kawaida tu unadhani ni hali ya kuzingatia sana hapana ni vile tu maisha yanavokuwa leo tunapata kesho tunakosa lakini hatupaswi kuacha kupambana ” maneno hayo yalimumiza sana. Tina akajikuta anamuonea huruma kelvin na haraka akaingis ndani na kuchukua kitenge chake na kumwambia kelvin ajifute maana alikuwa ana maugali ugali
MOYONI MWA TINA ……
huku akimfuta kelvin aliwaza “kelvin pole
kwa unayopitia pia nisamehe ni hasira tu jaman sikujua kama unapitia magumu hivi ” huku machozi yakimtoka kelvin akamuuliza unalilia nini sasa????
Tina alijibu “hapana hamna kitu kisha yeye akaingia ndani “
UPANDE WA ALICE
safari ya Alice baada ya kutoka kwa kelvin ilimchukua mpaka katikati ya bahari na hapo alikuwa nusu mtu nusu samaki (NGUVA) Alikuwa akitembea kama mshale mpake sehemu moja palipokuwapo na geti kisha alipoingia geti lilijifunga na akajikuta ametokea sehemu
nyingine (Sehemu hii inafanana na
sehemu ambayo kelvin aliiota kwenye ile ndoto )
Hapo alice alianza kuembea kwenda kwenye lile kasiri alikuwa ana miguu mizuri sana na muda huo alikuwa kavaa kichupi tu …….Kabla hajaingia dada yake kwa jina la sabrina alimwita
………..Aliceeeeeeeee!!!!¡!!!!!!!!!!!!;;;;;;
alionekana ana hasira sana
“hivi Alice mara ngapi una ambiwa usiende kwa binadamu ??? lakini wewe husikii ona leo kidogo ubadilike kuwa samaki mbele ya wanadamu si wangekuu wewe?? alisema sabrina …
“nisamehe dada nilihisi kelvin anahitaji
msaada wangu ndo mana nilienda ” allijibu Alice
” yaani sijawah ona watu wajinga kama wewe Alice hivi huyo kelvin una msaidia kwa nini kazi kumsaidia saidi ulimsaidia siku ile nymba yake ilikuwa ina waka moto sio hapo hata kwa rafiki yake Emanuel nako ulimsaidia pia ?? vipi umempenda au maana sio kwa shobo hizo ..
Alice alijibu “hapana dada siwezi kumpenda adui hata siku moja namsaidia hakuna mapenzi bhana niamnini “
haya sawa twende ndani ila cha msingi
kuwa makini na wanadamu unaweza kupoteza maisha ……… kisha waliondoka na kwenda ndani ya lile kasiri…
UPANDE WA KELVIN
Baada ya mvua kupungua tu alitoka na kuelekea maeneo ya sokoni ambapo alipofika huko alikuta na mzee ismail moja kati ya wateja wake wakubwa sana na mzee alipomwona alimpa pole kwa yote yaliyomkuta na kelvin alimwambia mzee anatakaa arejee mwanza akafanye mambo mengine lakini mzeee alimwambia hatakiwi kuondoka na kama hana nyumba yule mzee atampa nyumba
akae bure na hataki malipo yoyote yale
………….
Kelvin alifurahi san na kusema “hakika uishi maisha marefu mzee ismaili hakika wewe ni mwema kisha kelvin akapiga magoti mzee akamwinua na kusema wa kuabudiwa ni mungu na sio mimo mimi nimekusaidia wewr mwanangu kwa kuwa ulinisaidia mara nyingi kipindi sina hata mboga nyumbani kwangu …
NDUGU MSOMAJI CHA KUKUSIHI NI KWAMBA WEMA NI AKIBA NA UBAYA NI AKIBA UKIMTENDEA MTU MAMBO MEMA UTALIPWA MEMA UKITENDA MABAYA UTALIPWA MABAYA USISUBIRI JAMBO ULILOTENDWA ULIPWE HAPO HAPO
WEWE SONGA MBELE LAKINI JUA KUWA
UMEWEKA AKIBA NA AKIBA HAIOZI
.,………….. …………………
Lakini kumbe nyuma ya yote kuna binti alikuwa anamfuatilia alimpigia simu Goodluck na kumwambia kuwa kelvin yupo na ismaili Goodluck alimwambia aendelee kumfuatilia ajue wanataka kufanya nini ??? lakini alipomaliza kuja kuwatazama hakuweza kuona mtu walikuwa washaondoka
Alisema “wameenda wapi hawa watu
?????
Inaendelea
0 Comments