Walifika mbele wakapumzika walikuwa wamechoka sana, kama ni jini bado anawafata acha aje tu si kwa kuchoka huko. "Eva hata wewe umekimbia na si kukemea ulipaswa usimame" Ariana aliongea huku kichwani mwake akichora plan.
"Sema tu ni kitu gani hicho una fikiria " Eva aliuliza,
"Ndege kutoka China itaondoka hapa saa nane mchana, nahitaji kwenda China kupumzika ....nadhani hata kichambo cha Ex wangu nitakisahau. Na kitu cha kuvutia zaidi nitaisahau sura ya jini mzuri " Ariana aliomboleza.
"Kwani umeona maombi hayafai "
"Wee mwenyewe ulikimbia badala ya kukemea , sitaki kuwa mzigo kwako Eva wangu....ni kikaa mbali na huu Mji kwa siku kadhaa nitasahau mabalaa mengi, na jini mzuri hatakaa anifuate tena"
Basi kwa pamoja walikubaliana na hili kuwa itakapofika saa nane mchana Ariana aende China.
Upande mwingine, kukiwa kumepambazuka Yasin alipokea simu muhimu kutoka China,
"Itanilazimu kuondoka na ndege ya saa nane mchana" Yasin alijisemea huku akijiangalia kwenye kioo kwa uzuri aliokuwa nao yeye mwenyewe alijiogopa.
Hajamaliza kujiogopa simu yake iliita kwa mara nyingine tena.
"Daktari Ali niambie "
"Mmiliki wa hii baiskeli alikimbia akaiacha, mwenyewe ana wenge kama nini sasa sijui naiweka wapi "
"Niletee nyumbani kwangu, itanilazimu nimtafute mhusika kabla ya saa nane " Yasin aliongea kisha akakata simu, anaogopa sana kusononesha nafsi ya mtu.
Ndani ya dakika 20 aliweza kuipata baiskeli, alikuwa ni ya kishua haswa kiasi kwamba ina plate namba mfano wa gari.
Yasin ni mkorofi sana wa kucheza na mitandao, aliingiza plate namba ya baiskeli kwenye mtandao ndani ya dakika tatu majina ya Ariana yakiwa na sura yake aliweza kuiona.
"Kuna mtu nitampatia hii kazi, nahitaji kujiandaa kwa ajili ya safari " Yasin alijisemea kisha akashika karatasi alihitaji kumuomba msamaha mmiliki wa kibaiskeli.
Basi upande wa Ariana akiwa anajiandaa taratibu kwa ajili ya safari aliletewa taarifa.
"Baiskeli yako imeletwa " Eva aliongea huku akijiandaa kumdaka Ariana si anamjua ni hamnazo na ni mwepesi wa kuchanganyikiwa.
"Yule jini ndio kaleta baiskeli yangu hapa na ujumbe juu ?" Ariana aliuliza akiwa katika hali zote.
"Sijui lakini si ni ya kwako huna haja ya kuchanganyikiwa, nimeshaifunika kwa maombi " Eva alimtia moyo boss wake.
"Sawa....wacha nielekee uwanja wa ndege, nikiendelea kukaa hapa nitachanganyikiwa , Eva wa Mimi tutaonana wala hata usinisindikize kaa hapa uendelee kuizindika hii nyumba kwa maombi " Ariana aliongea kisha akaondoka, Dreva wake alimpeleka moja kwa moja hadi uwanja wa ndege.
Alikaa zaidi ya masaa tatu akiisubiria ndege. Kwa muda wote huo alikuwa anasikiliza nyimbo za dini asije kufuatwa na jini.
Baada ya ndege kufika abiria wote walitangaziwa kuchangamka.
Mmoja baada ya mwingine alikaguliwa .....
Ariana akiwa amepozi siti ya dirishani huku kafumba macho jirani yake alimsalimia.
"Habari yako Dada yangu "
Ariana alifumbua macho amuone mtu anaye msalimia . Kitendo cha macho yake kukutana na ya Yasin alizimia akiamini jini kamfuata hadi kwenye ndege.........
0 Comments