KAMDOMO TU KIUNO KIMEPOA POOH EPISODE 3

"Huyu ana shida gani kila akiniona anazimia " Yasin alijiuliza huku akimuita Mhudumu

"Kuna shida gani 🙄"

"Abiria huyu kapoteza fahamu...."

Bahati nzuri katika ndege hii kulikuwa na jopo la Madaktari wakienda China, Ariana alifanyiwa vipimo vya chapu chapu.

"Ni kitu cha kawaida tu, huenda ni mara yake ya kwanza kupanda ndege hivyo atakuwa sawa " Daktari bingwa aliongea.

Basi Yasin alikuwa mwema kwa kumuangalia Ariana.

Ndani ya dakika 40 alirejesha fahamu, pua zake zilipokelewa na harufu ya marashi ya Yasin.

Wacha aangue kilio 😭 kimya kimya, aliilaani ile siku aliyosema ni heri angeolewa na jini. Leo ndio alishtuka kuwa maneno huumba kuliko hata mikono ya mfinyazi.

"Unajisikiaje?..,tumia hii itakufanya uwe sawa " Yasin alimchangamkia huku akimpatia chocolate.

"Hii chocolate ni toleo la mwaka gani, mbona sijawahi kuiona tangu ni zaliwe au vinapatikana kwenye dunia yake tu " Ariana aliongea na moyo wake, mkono wake ulikuwa unatetemeka balaa, kwa shingo upande aliipokea chocolate.

"Eva yule jini kanifuata hadi kwenye ndege, inaonekana yeye pia anaenda China 😭 kazana kuniombea" Ariana alimtumia ujumbe Eva.

Eva si mtu wa kuwasha simu mapema hivyo ilimpa tabu sana.

"Unaenda China sehemu gani " Yasin alianzisha story.

"Ili unifuate " Ariana aliongea kwa kupaniki.
Watu waliokuwa wamekaa jirani yao walimgeukia.

"Dah ndio nishaanza kuonekana hamnazo CV yangu inashuka sababu ya huyu jini mbwa " Ariana alilalamika ndani ya moyo wake huku akijitahidi kujiweka sawa.

"Bila shaka ana wakati mgumu huyu, siwezi kumuacha hivi 😊" Yasin alijisemea kisha akashika simu yake. Alimtafutia Ariana movie ya kuchekesha kisha akamkabidhi simu.

Ariana alitaka kuisukumiza kule lakini kuna sauti ilimuambia.

"Oyaaah, ukiendelea kumuonesha huyu jini kiburi itakula kwako "

Afanye nini sasa, aliendelea kutazama movie..... vile inachekesha sasa alijikuta akicheka. Wacha akosee amgeukie Yasin, macho yao yakakutana alitamani kupiga kelele. Jicho la Yasin lilikuwa jeupe peee na kubwa.

"Naweza kujua ni kitu gani kina kusumbua? japo sina cheti lakini nipo vizuri kwenye kushauri " Yasin alizidi kujipendekeza.

Kabla Ariana hajatoa jibu ujumbe uliingia kwenye simu yake. Kutoka kwa Eva.

"Ongea naye tu, angekuwa ni jini watu wengine wasingekuwa wanamuona na kitu cha kufurahisha kabisa wakati ukaguzi unafanyika ili muingie kwenye ndege asiongeonekana kwenye mashine " Ujumbe wa Eva ulimtia moyo Ariana.

"Shika hiki kitambaa ujifute jasho, unaonekana unapitia mengi moyoni mwako pole sana " Yasin aliongea kwa sauti ya kubebembeleza.

"Hili nalo ni jaribu, huenda huyu jini anajifanya Eva na anaanza kulaghai akili yangu taratibu " Ariana aliongea pekee yake huku akijifuta mijasho iliyokuwa jnatiririka usoni.

Yasin naye king'ang'anizi aisee alizidi kulazimisha urafiki . Aliomba namba huku akijichekesha hivi.

Ariana akiwa mwenye machungu aliandika namba zake zote nne. Alifanya basi tu kuepuka kutafunwa.

"Kwahiyo unaenda China sehemu gani?....."

"Hong Kong "

"Oh Mimi pia naenda Hong Kong, kuna bidhaa muhimu sana naenda kufuatilia " Yasin aliongea huku akitabasamu.

Tabasamu lake lilikuwa la kipekee sana, moyo wa Ariana ulidunda kupita kiasi.

"Kwanini nisimuulize kuhusu familia yake,?" Ariana alikusanya ujasiri kisha akamuuliza.

Wacha apagawe baada ya kuiona familia ya Yasin..... walikuwa ni wazuri haswa.

"Tupige picha moja ya ukumbusho tafadhali 😊" Yasin alipendekeza.

Ariana hakuweza kukataa, ile wanaweka kitu cha selfie 🤳 Yasin mwenyewe alijiogopa 🤣 hakuamini kama yeye ni mwenye kuvutia namna hii kupita kiasi.

Aliiziba sura yake kwa kuweka mkono, Ariana wa watu aliamini huenda hili ni pozi. Yeye pia alifanya kuiga kwa kuiziba sura yake na mkono.........

Picha ilifotolewa chwaaaaaa............

Jirani eeeh yajayo yanafurahisha 👌..........

ITAENDELEA.........

Post a Comment

0 Comments