THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI) - EPISODE 01

 


Mama mdogo mimi nimechoka na haya maisha haiwezekani kila siku ninapoteza pesa zangu. Nimeshagombana na watu wengi sana nikiwatuhumu kwamba nichuma ulete. Haya usiku wa jana, nilikuwa na shilingi laki mbili na elfu ishirini, nilikupa elfu ishirini cha ajabu pesa niliyoiweka kwenye wallet yangu haionekani. Kwa nini mimi?. Ni lazima kutakuwa na mtu ananifanyia mchezo mchafu. Mama mdogo alisema mimi nina mashaka na yule mkeo uliyemfukuza.

Kama unakumbuka viziri kipindi uko na mke wako pesa zilikuwa hazipotei kimazingara. Ni lazima atakuwa ni mke wako. Eti mama mdogo alisema Kelvin huku akinyanyuka kwenye kiti.


 Hebu kaa kwenye kiti unataka kwenda wapi?. Mama si nataka nikawatembelee rafiki zangu. Sikia mimi nataka nikupeleke sehemu. Sehemu gani?. Mimi nataka nikupeleke kwa mtaalamu.

"Mtaalamu"

"Mtaalamu gani?"

Aliuliza Kelvin huku akiketi kwenye kiti. Nitakupeleka Kwa Mzee Nungunungu, wewe mama mdogo mbona sikuelewi, huyo mzee Nungunungu wa kazi gani?. Mmh!!!, kijana wangu kumbe bado haujakua, unaniuliza maswali gani hayo. Sikiliza Mzee Nungunungu atakusaidia matatizo yako yote, na hiyo biashara unayosema eti imekuwa mbaya mtaalamu atakutengenezea dawa ya biashara haya kama ni kuhusu pesa kupotea hazitapotea tena.


 Umenielewa mwanangu. Mama mimi nimekuelewa ila bado ninaswali hivi kweli huyo mtaalamu wako atanisaidia. Ndio lazima atakusaidia hiyo ni kazi ndogo kwake. Kweli mama mdogo. Wewe jiandae twende nikupeleke. Sawa mama mdogo.


Hodi hodi wenyewe. Pita ndani, vueni viatu vyenu sawa. Sawa mtaalamu. "Pakacha!!!", pakachaaa!!!, Pukuchuu!!!, Pukuchuuu!!! ". Baada ya Mzee Nungunungu kuimba nyimbo zake alivuta pembe la ng'ombe kisha akaanza kulipuliza lile pembe huku akirudia kuimba zile nyimbo zake," Pakachaa!!!!, pakachaaa!!, Pukuchuu!!!!, Pukuchuu!!! ". 


Mzee Nungunungu alisema kijana pole sana na matatizo ila hapa ndio mwisho wa reli. Asante babu, ila unamaanisha nini?. Teh!!.. tehee!!!, baada ya kumaliza kucheka akamwangalia mama yangu mdogo. 


Vipi Zubeda haujamwambia taarifa zangu. Nilimwambia lakini sijui bado hajaamini,alisema mama mdogo huku akininong'oneza kwamba pale siruhusiwi kuuliza maswali. Sasa kijana hapa ndio mwisho wa shida zako, hebu leta mkono wako. Baada ya yule Mzee Nungunungu kuutizama ule mkono alianza kusema una bahati sana, tena inakupasa umshukuru sana Zubeda.


 Zubeda huyu si ni mtoto wa dada yako. Ndio Mzee Nungunungu. Sasa aliyemfanyia mchezo mchafu katika biashara zake na hata kupotea kwa pesa zake ni Deborah. Huyu mke wangu Deborah Josephat aliuliza Kelvin. 


Ndio, alisema Mzee Nungunungu huku akilishika pembe la ng'ombe. Nilijua tu, alisema mama mdogo huku akinipiga kwenye bega la kulia.


Mama nitaua, nitaua mtu. Sikia kijana huna haja ya kuua, kuna njia mbadala ambayo utatakiwa uifanye na sio kumuua Deborah. Njia ipi?,aliuliza Kelvin huku akiwa ameshika shavu la kushoto. Nitakupa hizi dawa, ukishazitumia hizi dawa kila kitu kitaenda sawa. 


Uko tayari nikupe maelekezo ya hizi dawa. Ndio niko tayari. Sikiliza kwa makini hii dawa utakuwa unaweka kwenye maji ya kuoga kisha unaoga asubuhi na jioni, sawa. Sawa Mzee Nungunungu. Halafu hii dawa iliyokwenye mfuko mwekundu ni mfupa wa simba. Utakuwa unawahi asubuhi sana kwenye duka lako la mchele kisha unachimba pembezoni mwa duka lako na kuweka hii dawa. Hakikisha mtu asikuone wakati ukichimba, ukishamaliza kuchimba unafukia. Ikifika usiku wa manane unaitoa pale kwenye shimo.



 Utafanya hivyo kwa muda wa siku saba, Umenielewa. Nimekuelewa Mzee Nungunungu, ila ninaswali nitaoga hii dawa kwa siku ngapi?,lakini pia huu mfupa wa simba nitakuwa ninauweka dukani kipindi nikifunga duka langu au laa. Hiyo dawa utaoga asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba, halafu kuhusu huu mfupa wa simba pindi unapoutoa pembezoni mwa duka lako  itatakiwa ulale nao kitandani.


 Kitandani!!!?, alisema Kelvin. Mzee Nungunungu akajibu ndio lazima ulale nao tena ukiwa umeukumbatia huo mfupa wa simba. Maana yake ni kwamba unakuwa umekumbatia wateja wote. Ukifuata masharti utafurahi mwenyewe, ila usipofuata masharti kuna hatari kubwa ya mizimu yangu kukufanya kitu kibaya.


****

Angelina Bernard alikuwa nchini Israel akiendelea na masomo yake, mara nyingi alijiona mpweke Sana. Maana hakuzoea mazingira ya pale Israel ukizingatia alitamani sana shahada yake ya udaktari akasome katika nchi ya India. Kila muda alikuwa akimpigia simu baba yake na kumsihi amuhamishe chuo cha kikuu cha Israel ampeleke katika chuo kikuu kilichokuwa India. 


Baba yake alikuwa mkali sana, aliendelea kumwambia Angelina tafadhali usinipe ugonjwa wa moyo kama hautaki kusoma sema. Hicho chuo kikuu cha Israel mbona kina maprofesa waliobobea katika fani ya udaktari. Mimi siko tayari kukuhamisha chuo sawa. 


Lakini baba. Lakini nini?. Mzee Bernard alikata simu. Binti yake alijaribu kupiga simu lakini haikupokelewa tena. Huyu baba kwanini ananilazimisha mimi.

" Sitaki"

"Nimesema sitaki"

Wewe Angelina mbona hivyo kama haumtaki George ndio uanze kutupigia kelele. Kila muda "sitaki!!, sitakii!!, umetuchosha na kelele zako.Tutakuita "staki nataka"


 Pwaaaa, lilikuwa nikofi alilopigwa Getruda na kudondoka chini. Mshenzi sana unajifanya kuingilia mambo yasiyokuhusu. Mimi ninampigia baba yangu anihamishe chuo, halafu wewe unakuja kunambia habari za George. Angelina alishtuka hii ni baada ya kuona Getruda bado amelala pale chini. Wewe Getu.... Getruda.... Getrudaa!!!!.


ITAENDELEA...... 

Je, Kelvin ataweza kufuata masharti ya mtaalamu Nungunungu lakini pia Angelina Bernard amempiga kofi Getruda lakini Getrudaa amelala chini ili kujua kama Getruda amepoteza fahamu au amekufa usikose kufuatilia Sehemu ya Pili ya hadithi yako nzuri ya THE DEVIL TONGUE(ULIMI WA SHETANI) 

Post a Comment

0 Comments