Wewe binti unauwezo mzuri sana, umesomea kozi ya utabibu maana umeweza kumsafisha vizuri na kushona kidonda huyu mgonjwa. Baba mimi ninaomba umpatie ajira inaonekana anauzoefu na hii kazi. Angelina alijibu kawaida tu. Hapana hii sio kawaida, alisema mmiliki wa hospitali huku akimsihi Angelina kuleta vyeti ili amwajira katika hospitali ya MFALME SULEIMAN. Angelina alijifikiria kidogo kisha akaamua kudanganya kwa kusema kwamba
"Sina vyeti" ,
"Vyeti vyangu vilipotea".
Duuh!, pole sana. Ila baba mimi ninaomba umuajiri hivyohivyo bila vyeti. Wewe binti yangu Catherine mbona unaongea sana. Hapana baba mimi nimependa jinsi Angelina anavyochapa kazi. Sawa nitamuajiri. Asante baba, alisema Catherine huku akimshika mkono Angelina na kumwambia furahi umeshapata kazi kwenye hospitali ya baba yangu. Wakati wameshikana mikono. Ghafla Dr Suleiman alimshtukiza Angelina Kwa kumuuliza maswali haya.
"Una miaka mingapi?"
"Na hapa Israel unaishi sehemu gani?"
Angelina alijibu swali la kwanza, kwa kusema ninamiaka 23. Swali la pili lilikuwa gumu kujibu maana Angelina alianza kulia tu. Tafadhali nyamaza usilie. Catherine alimtuliza. Muda wote Dr Suleiman alikuwa akijiuliza maswali Kwanini Angelina analia. Angelina aliongea huku akilia,mimi na wazazi wangu tulikuja kutalii katika nchi ya Israel kwa bahati mbaya siku tunatoka uwanja wa ndege tulipanda tax, tukiwa njiani tukapata ajali mbaya sana, mimi tu ndiye nilisalimika katika hiyo ajali. Pole Dada. Pole binti yangu. Walisema wote huku wakimuonesha mazingira ya ile hospitali.
Kila siku wagonjwa waliongezeka katika hospitali ya "MFALME SULEIMAN". Wewe binti sijui nimekufananisha. Kwa nini unasema hivyo. Tizama hii picha, huyu mtu aliyekuwa kwenye picha unafanana naye sana halafu anatafutwa na polisi. Hapana kaka utakuwa umenifananisha. Baada ya yule kaka kuondoka Angelina hakuwa na amani alibaki akiwaza juu ya kutafutwa na polisi akiwa katika dimbwi la mawazo akajikuta akilitaja jina la Dickson.
****
Wasamaria wema waliwabeba Kelvin na yule bodaboda. Japo hali zao zilikuwa mbaya lakini walipelekwa hospitali ya Mwananyamala. Walipelekwa moja kwa moja mpaka chumba cha uangalizi maalumu(ICU). Zubeda alikuwa ameshafika kumwona kijana wake. Alijikuta akimuuliza Daktari maswali mfululizo.
"Mwanangu anaendeleaje?"
"Mwanangu ni mzima au amekufa?".
Daktari alimwambia yule mama awe mpole mgonjwa wake bado anapewa matibabu. Madaktari wa siku hizi wanajibu "shortcuts" hii ni kwa sababu hawajui uchungu wa kuzaa, alisema Zubeda huku akikaa kwenye viti vya mapokezi.
Huyu naona damu yake imevujia kwenye ubongo alisema Daktari Rwechungura huku akiwaongoza madaktari wenzake katika kumfanyia upasuaji yule mgonjwa. Daktari Rwechungura alitikisa kichwa baada ya kugundua kwamba upande mmoja wa mwili wa Kelvin umepooza. Mbona umetikisa kichwa kuna tatizo lolote, waliuliza madaktari wenzake. Ndio huyu mgonjwa hataweza kutumia mkono wa kulia wala mguu wa kulia. Kwa hiyo unamaanisha huyu mgonjwa amepooza upande wa kulia. Ndio, ila bora tumeokoa uhai wa huyu mmoja, maana huyu mwenzake ameshafariki. Baada ya yale mazungumzo daktari alichukuwa sindano kisha akamchoma Kevin sindano ya usingizi. Tumwache apumzike alisema Dr Rwechungura huku akipiga hatua za kuaelekea nje ya ICU.
Daktari afadhali nimekuona, hebu nambie mwanangu Kelvin anaendeleaje?. Wewe ni nani yake aliuliza Dr Rwechungura huku akivua miwani yake. Mimi ni mama yake mdogo. Sawa nifuate ofisini. Baada ya kufika ofisini, daktari Rwechungura alimkaribisha kiti Zubeda. Lakini Zubeda alikataa kata kukaa mpaka aambiwe taarifa za Kelvin. Sawa nitakwambia iko hivi kijana wako Kelvin anaendelea vizuri ila kuna changamoto kidogo. Changamoto ipi alisema Zubeda huku akijifunga vizuri kitenge chake. Daktari Rwechungura alikohoa kidogo kisha akasema mwanao amepooza upande wa kulia. Zubeda alisema
"Amepooza!!!"
"Unamaanisha Kelvin amepooza"
Ndio,alisema Daktari huku akivaa miwani yake. Ninaweza kwenda kumwona. Hapana. Wewe daktari mbona hivyo. Au unanificha mwanangu ameshakufa. Kwanini unanizuia nisiende kumwona mwanangu. Nimekwambia "hapana" kwa nini hutaki kuelewa alisema daktari Rwechungura huku akigonga kwenye meza kwa hasira. Ilimbidi Zubeda aondoke ofisini kwa daktari huku akimkata jicho.
Baada ya siku mbili kupita Kelvin alipewa ruhusa ya kutoka hospitali ya Mwananyamala. Wakati Daktari Rwechungura akimpa Zubeda maelekezo, Kelvin alikuwa amejiinamia huku machozi yakimtoka. Bahati nzuri Daktari aligundua akaamua kumpa ushauri Kelvin kwa kumwambia kwamba ;
"Ulemavu sio mwisho wa maisha"
"Usijutie kuwa mlemavu"
"Ulemavu ni hali ya kawaida"
Daktari aliongezea kwa kusema kuna watu wanazaliwa wakiwa walemavu lakini hawajutii na wala hawajikatai. Mshukuru sana Mungu wa mbinguni maana wewe uko hai lakini bodaboda uliyekuwa naye amefariki. Kelvin alilia kilio cha kwikwi huku akisema bora na mimi ningefariki. Hapana, hapana. Usiseme hivyo Kelvin utamkufuru Mungu. Daktari alimfuta machozi huku akisaidiana na mama mdogo kuniweka kwenye gari kwa ajili ya kurudi nyumbani.
Baada ya kufika nyumbani, mama mdogo aliandaa chakula. Mimi nilibaki chumbani kwangu huku nikitafakari maisha mapya ya ulemavu. Nikiwa katika dimbwi la mawazo nilishtuliwa na mlio wa simu. Sijui atakuwa nani?,nilijisemea huku nikijaribu kuishika simu yangu kwa mkono wa kushoto. Nilitizama na kuona namba ngeni. Nilitaka kupuuzia kupokea lakini Baada ya kujifikiria Kwa sekunde kadhaa nikaamua kuipokea ile simu. Haloo, sauti ilisikika kutoka kwenye ile simu. Kaka mbona kimya sana. Kelvin akauliza wewe ni nani?. Kigosa hapa mkulima wa mchele, si ulipiga simu kwamba nikuletee mchele, sasa kwa kuwa nilikuwa bize nikaamua kutuma vijana wangu wakuletee mchele. Vipi mzigo umefika. Kabla Kelvin hajajibu ghafla simu ikazima. Shiit!!, simu imeisha chaji. Mbona hii simu sijaielewa. Nahisi atakuwa amekosea namba.
Mama mdogo alileta chakula nilikula lakini nikiendelea kutafakari ile simu niliyopigiwa. Mama mdogo aliendelea kunisihi nisiwe na mawazo hata kidogo huku akinipa mifano mbalimbali. Baada ya kumaliza kula mama mdogo alinambia kwamba ule mfupa wa simba alienda kuutoa dukani kwangu. Kwa hiyo uko humu chumbani kwangu. Ndio alijibu mama mdogo huku akinionyesha kwa kidole kwamba nikifunua mto wa kulalia nitauona ule mfupa wa simba. Baada ya mama mdogo kunambia aliniaga na kuondoka. Kwa kuwa nilikuwa katika hali ya ulemavu niliamua kuutupa ule mfupa wa simba katika uvungu wa kitanda, kutokana na uchovu nilipitiwa na usingizi.
Nilikuja kushtuka usiku wa manane nikisikia mabundi yakilia sana, lakini nilipojitazama kwenye miguu yangu niliona moto ukiwaka. Nilijiuliza moto unawaka kwenye miguu yangu halafu mimi sisikii maumivu yeyote. Halafu sehemu zilizobakia nilikuwa nikipuliziwa perfume ila perfume ya safari hii ilikuwa ikiniwasha utafikiri nimemwagiwa maji ya upupu. Nilijikuna mwili mzima kilichonishangaza kila nilipokuwa ninajikuna walikuwa wakitoka funza katika mwili wangu.
ITAENDELEA.........
Je, Angelina atakamatwa na jeshi la polis lakini pia ni kwanini Angelina amelitaja Jina la Dickson. Upande wa pili Kelvin anajikuna na mwili wake unatoa funza baada ya kujikuna. Ili kujua yote usikose kusoma sehemu ya 5 ya hadithi yako nzuri ya "THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI).
0 Comments