THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI) - EPISODE 03

 

Wakati nikiendelea kujikuna mama mdogo alinistua, wewe Kelvin amka uwahi kuoga ile dawa halafu uwahi kuufukia mfupa wa simba katika duka lako la mchele. Nilijikuta nikiropoka mfupa wa simba?. 
"Mbona mimi nina perfume" 
"Sina mfupa wa simba". 
 Hebu acha masihara amka ujiandae. Wakati nikitoa ile shuka nilishangaa kuona ile perfume ikibadilika na kuwa mfupa wa simba. Nilitaka kupiga kelele lakini nilipofungua mdomo wangu ulikuwa mzito. Sikuweza kabisa kupiga kelele, ilinibidi niamke nijiandae kwenda kuoga ile dawa kisha nilichukuwa mfupa wa simba nikaanza safari ya kuelekea Mbagala rangi tatu.


 Baada ya kufika kwenye duka langu nilichimba shimo dogo nikaweka ule mfupa wa simba kisha nikaufukia.
Nilifungua duka langu kisha nikaingia na kuanza kupanga vizuri magunia ya mchele. Daah!, imekuwa kama bahati kumbe saa kumi na mbili asubuhi mnakuwa mmeshafungua maduka. Hapa nilikuwa ninawaza sana kuhusu mchele na maharage. Umepata mteja wangu. 
"Karibu Sana". 
"Asante sana. 
Ulikuwa unahitaji kilo ngapi za mchele na maharage?. Nipatie kilogram 50 za mchele na kilograms 30 za maharage. Kilichomshangaza Kelvin ni pale yule mteja alipoanza kutoa pesa bila hata kuulizia bei ya mchele na maharage. Wala hata hakutaka kuangalia kama mchele ni mzuri au mbaya.


Kelvin alimaliza kupima akapewa pesa shilingi laki moja na elfu hamsini. Mteja wangu jumla ni shilingi laki moja na elfu arobaini na tano. Mteja alicheka kisha akasema ninajua kwamba elfu tano imezidi ila nimeamua kukuachia ili unywe soda. Asante sana. Yule mteja aliita kirikuu kisha ikabeba mchele na maharage. Wateja waliendelea kuongezeka mpaka inafika saa tisa alasiri Kelvin alikuwa amemaliza mchele na maharage. Wafanyabiashara wenzake walikuwa wakijiuliza huyu Kelvin
"Mbona anauza sana.
"Sisi hatujauza hata mia". 
Lakini wewe uko bize kupima tu. Hebu tueleze vizuri. Kama vipi tukuuzie huu mchele wote ili uuze peke yako.


 Washikaji zangu mnazingua tena mnazingua kinoma. Kipindi ninyi mlipokuwa mkiuza mbona nilikuwa silalamiki, hebu acheni lawama zisizo na kichwa wala miguu. Hata kama Kelvin haiwezekani uuze zaidi ya kilograms mia sita za mchele sisi tunakutazama tu, hapa kuna kitu sio bure. Kelvin aliamua kuepusha shari akalazimika kufunga duka lake na kuelekea nyumbani japo alikuwa na furaha lakini hakuwa na amani. Maana kitendo cha kuuza mchele wote na maharage kilitengeneza uhasama kwa rafiki zake. Watajua wenyewe kwani nimewazuia kwenda kwa Mzee Nungunungu, alijisemea Kelvin wakati akifungua mlango wa chumba chake. 
Mama yake mdogo alimuita Kelvin na kumuuliza mwanangu vipi leo biashara usinambie kwamba biashara bado ni mbaya. 

Mama mdogo yule Mzee Nungunungu ni hatarii. Ile dawa imepiga kazi. Huwezi amini nimeuza kilograms mia sita za mchele na kilograms mia nne za maharage, tena imefika saa tisa alasiri nikawa nimeshamaliza kuuza. Mama mdogo alinikumbatia na kusema huo ni mwanzo tu, mwaka huu lazima utajirike. Ila mama mdogo rafiki zangu wamenichukia sana. Achana nao, alisema mama mdogo huku akinisihi saa nne usiku nikumbuke kwenda kuufukua ule mfupa wa simba ambao ulikuwa pembezoni mwa duka langu. Sawa mama mdogo nitafanya hivyo.
Ilipofika saa nne usiku Kelvin alichukua bodaboda kutoka Tandika mpaka Mbagala rangi tatu. Wakati wameanza safari ya kutoka Tandika walipofika Mbagala kwa Azizi Ally kuna bus lilifeli breki likawagonga. Zilisikika kelele mmeua!!!,mmeuaaa!!!!


****
Baada ya Angelina kupata fahamu alijikuta akiuliza maswali mfululizo hivi ni kweli nimeua lakini pia ni kweli wazazi wangu wangu wamefariki au niko kwenye ndoto. Inawezekana vipi wazazi wangu wapoteze maisha halafu wazikwe bila mimi kupewa taarifa. Angelina alijikuta akiangua kilio. Mpaka wauguzi waliokuwa katika ile hospitali walijiuliza kwamba Angelina amepatwa na kichaa . Muuguzi mmoja alimsogelea kisha akamwambia kwamba asiwe na hofu pale ni sehemu salama. 


Angelina baada ya kutoka hospitalini alipelekwa mahakamani kesi yake ikasikilizwa. Kwa kuwa Angelina alikiri kosa. Muda huohuo Hakimu Boniventure Paulsen, alimuhukumu Angelina kifungo cha maisha. Angelina aliyaanza maisha mapya ya gerezani. Katika maisha yake aliamini kabisa mtu aliyekuwa jela lazima alikuwa Jambazi au mbakaji. Lakini safari hii alijishangaa kwamba yeye naye amekuwa mfungwa kwa kosa la kuua. Alijikuta akiweka mkono shavuni huku machozi yakimtiririka alijisemea kimoyomoyo hivi kweli niko jela.
Angelina akiwa gerezani afya yake ilianza kuzorota hii ni baada ya kukataa kula huku akisema kwamba ni bora afe kwa njaa kuliko kula chakula cha gerezani. 

Kulipopambazuka Angelina hakuwa katika lile gereza, hii ilikuja kujulikana baada ya wafungwa wenzake kuamka na kukuta hawana titi la kushoto. Kila mfungwa alikuwa akishika kwenye kifua kisha anapapasa titi la kushoto anakuta titi halipo. Mkuu wa magereza alishangaa sana kupata zile taarifa za wafungwa kukatwa titi la kushoto.Aliuliza ni askari gani alikuwa zamu usiku .Ni mimi hapa Mkuu. Sasa Afande Zakayo ulikuwa wapi, mpaka Angelina akawakata titi la kushoto  wafungwa wenzake. Mkuu nisamehe, nilipitiwa na usingizi. Wewe Afande Zakayo kutokana na uzembe uliofanya utakaa humu jela mpaka Angelina apatikane. 


Boss nisamehe. Hakuna cha msamaha hapa,  Afande Patrick sukuma ndani huyo Afande Zakayo. Sawa mkuu alisema Afande Patrick na kumuweka sero afande Zakayo.  Mkuu wa magereza alitoa amri kwamba inatakiwa Angelina atafutwe kila kona. Ninawapa saa 24  huyo Angelina awe ameshakamatwa haraka sana. Sawa mkuu waliitikia askari na kuondoka.


ITAENDELEA...


Je, Kelvin amepoteza maisha baada ya kupata ajali au laa. Upande wa pili Mkuu wa magereza anatoa amri kwamba Angelina atafutwe kila kona. Hii ni baada ya kukuta Angelina hayumo gerezani lakini cha ajabu wafungwa wote walikuwa wamekatwa titi la kushoto. Ili kujua nini kitaendelea usikose kusoma hadithi ya THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI) EPISODE YA 04.

Post a Comment

0 Comments