THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI) - EPISODE 02


Kuna nini mbona Getruda yuko chini. Diana mimi nilikuwa nimemaliza kumpigia baba yangu simu. Sasa baba akawa amekataa kunihamisha chuo. Getruda akanikuta nikisema sitaki, nimesema sitaki, kwa kuwa hakujua kama nimetoka kuongea na simu. Muda huohuo akaanza kunambia kwamba "wewe Angelina, mbona hivyo kama haumtaki George ndio uanze kutupigia kelele, kila muda sitaki sitaki, umetuchosha na kelele zako" . Nilivyosikia hivyo nikakasirika sana nikajikuta nimempiga Kofi moja, moja tu wala sijampiga kofi lingine, cha ajabu Getruda alianguka chini na kukaa kimya. Sijui amepoteza fahamu, alisema Angelina huku akitetemeka kwa woga. Diana alisogeza sikio kwenye kifua cha Getruda.


 Baada ya kusogeza sikio lake akabaini kwamba Getruda ameshapoteza maisha. Huyu amekufa. Unamaanisha Getruda amekufa. Ndio. Mungu wangu!!!!. Si nitafungwa, tafadhali Diana ninaomba usiseme chochote. Ni lazima niseme, tena ngoja nimpigie simu matroni. Baada ya Matroni kufika alishangaa sana baada ya kuelezwa jinsi Angelina alivyofanya ukatili wa kukatisha maisha ya Getruda. Wewe Angelina umeanza lini kuwa bondia. Hapana Matroni mimi sio bondia, ni bahati mbaya tu, wala sijakusudia tafadhali nisamehe. 


Ninaapa kwa Mungu wangu mimi nilimpiga kofi moja, moja tu, wala sijamsukuma, alidondoka mwenyewe. Wewe Angelina kwa ukatili uliofanya ni lazima ulipe. Matroni alimpigia simu mkuu wa chuo kisha akapiga simu polisi. Baada ya polisi kufika waliubeba ule mwili wa Getruda, kisha walimfunga pingu Angelina nakumrusha kwenye difenda. Muda wote Angelina alikuwa akilia kama mtoto mdogo huku akiomba msamaha. 


Haya sema haraka majina yako alikuwa ni Afande John Franco si ninakuuliza wewe unachezea jeshi la polisi, si ndio. Hapana Afande. Haya nambie majina yako. Ninaitwa Angelina Bernard nimetokea Tanzania. Una wazazi au umeshawaua maana wewe ni bingwa wa kuua. Ndio ninawazazi. Haya nipe namba za simu za baba yako. Baada ya Angelina kutaja namba za simu za baba yake.


 Yule Afande Franko alianza kupiga zile namba lakini zilikuwa hazipatikani, alijaribu tena kupiga lakini bado simu ilikuwa haipatikani. Wewe binti umenipa namba za gari mbona kila nikipiga hizi namba hazipatikani. Ndio namba za baba yangu. Afande hebu jaribu kupiga hizi namba za mama yangu. Hebu weka mwenyewe kwenye simu yangu. Baada ya Angelina kuweka zile namba za simu ya mama yake, lakini bado simu Ilikuwa haipatikani. Umeona eeh!!, usifikiri unanikomoa, unajikomoa mwenyewe. Mimi nilitaka kuwapa taarifa wazazi wako, wewe unajifanya jeuri kwa kunitajia namba za magari. 


Namba nilizotaja ndizo za wazazi wangu wala sijakudanganya. Basi ngoja nikutajie namba za simu za shangazi yangu. Wewe binti mimi sina muda wa kupoteza sawa. Jamani Afande tafadhali. Kuna nini hapa?, aliuliza ACP Joseph Metthew. Aah!!!, huyu binti analeta jeuri namwambia anitajie namba za wazazi wake, lakini yeye ananitajia namba za magari. Namba za magari!!!!?. Ndio. Hapana Afande alisema Angelina  huku akilia kilio cha kwikwi. ACP Metthew alimsogelea kisha akamwambia hebu nitajie namba za simu za wazazi wako. Angelina alifuta machozi kisha akasema namba za baba hazipatikani ngoja nikutajie namba ya shangazi yangu. Haya hebu, mpigie kwenye hii simu yako. Baada ya Angelina kupewa simu yake alianza kutafuta majina kwenye simu yake kisha alipiga ile namba ya shangazi yake. ACP Metthew alimkwapua ile simu Angelina na kisha akasema mbona inaita tu. 


Upande wa pili, mama. Dada Angelina amepiga simu. Wewe ni muongo, au umeshamwambia kilichotokea. Akhaa!!!, sijamwambia chochote. Kapiga mwenyewe simu, mama si upokee jamani. Wakati shangazi yake Angelina akijifikiria kupokea simu. Ghafla Yunia alimkwapua simu mama yake kisha akaipokea. Haloo..., mimi ni ACP  Kutoka kituo cha polisi cha Israel. Yunia alijikuta akiropoka Polisi!!!!. Ndio, huyu binti yenu anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji. Mauaji!!!!?,mama hebu shika hii simu uongee na huyo askari mimi simuelewi naona ananichanganya. Baba yangu binti yangu amefanyaje?. Binti yako Angelina Bernard amekutwa na kesi ya mauaji. Mungu wangu. Naweza nikaongea naye alisema shangazi huku akilia. 

Wewe Angelina,

 Abee shangazi.

 Umefanya nini?. 

Shikamoo shangazi. Marahaba haya nambie ukweli. Ni kweli umekutwa na kesi ya mauaji. Ndio, shangazi ila ni bahati mbaya tu. Halafu kwanini Baba na mama yangu hawapatikani au baba amechukia tangu nilipoongea naye ili anihamishe chuo. Sio hivyo binti yangu. Kwanza pole kwa yaliyokukuta ila kusema ukweli wazazi wako wote walipata ajali na kupoteza maisha. Angelina alisema "Wee!!!, shangazi" kisha akaanguka chini nakupoteza fahamu.


****

Ukifuata masharti utafurahi mwenyewe, ila usipofuata masharti kuna hatari kubwa ya mizimu yangu kukufanya kitu kibaya. Sawa Mzee Nungunungu nimekuelewa na niko tayari kufuata masharti. Mama mdogo si tuage ili tondoke alisema Kelvin. Mama mdogo aliniziba mdomo wangu na kuninong'oneza kwamba hapa huwa hatuagi, tunaondoka kimyakimya tena haturusiwi kugeuka nyuma. Nilijikuta nikitikisa kichwa kama ishara ya kukubali kisha tulianza safari ya kuondoka kwa mtaalamu Nungunungu.


Baada ya kufika nyumbani nilianza kufanya kama nilivyoagizwa na Mtaalamu Nungunungu. Sitasahau usiku nilipokuwa nimelala, nilisikia sauti za wanyama nilifumbua macho na kukuta ule mfupa wa simba  niliyokuwa nimeukumbatia umebadilika na kuwa kitu cha kutisha. Nilishangaa kuona mtu akiwa ana kichwa cha simba, pia niliona jogoo wawili wakiwa hawana manyoya. Niliogopa sana baada ya kuona vile. 


Ghafla yule mtu aliyekuwa na kichwa cha simba alitoweka pia wale jogoo wawili waliwika kisha wakatoweka. Nilitamani kukimbia lakini mwili wangu ulikuwa kama umepigwa ganzi. Muda huohuo ule mfupa wa simba uligeuka na kuwa uturi(perfume), kisha nikashangaa nikipuliziwa perfume mwili mzima.

"Nilijiuliza ni nani?". 

"Anayenipulizia perfume". 

 Niliangaza kila sehemu ya chumba changu lakini sikufanikiwa kumuona mtu yeyote . Ghafla ile perfume ilianza kuniwasha mwili mzima. Nilijikuta nikianza kujikuna huku nikilia na kujuta.


ITAENDELEA........... 

Je nini kitamkuta Angelina Baada ya kupoteza fahamu. Upande wa pili Kelvin anapuliziwa perfume inayomuwasha mwili mzima na anayempulizia perfume Kelvin haonekani. Je nini kitaendelea kwa Kelvin. Usikose kufuatilia episode ya 03 ya hadithi yako nzuri ya THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI). 

Post a Comment

0 Comments