Ghafla mlango ulifunguliwa akaingia askari mmoja mrefu sana. Angelina aliendelea kulia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata. Angelina alisikia mazungumzo kati ya yule askari mrefu na wale askari wawili akabaini kitu kisha akasema aliyefanya huo ukatili nimemkumbuka ni Afande Dickson. Unasemaje, waliuliza wale askari wawili. Afande Dickson hawezi kufanya huu upuuzi. Wewe ni muongo alisema askari mmoja huku akiendelea kumpa mateso Angelina.
Afande Dickson amekuja hapa kufanya mazoezi ya vitendo(field) na kumbuka Afande Dickson ni mwanafunzi ambaye amekuja kujiendeleza kielimu katika chuo cha mafunzo ya uaskari hapa nchini Israel, hawezi kufanya huo upuuzi. Nakuapia kabisa aliyenyuma ya haya yote ni Afande Dickson. Yule askari mrefu alimzuia askari mwenzake. Tafadhali acha kumpa mateso. Huyu ni muuaji mkubwa anastahili adhabu. Uko sahihi Afande, alisema yule askari mrefu huku akimsogelea Angelina. Angelina kwanini unasema Afande Dickson ndiye amehusika kuwakata wafungwa titi la kushoto. Iko hivi afande. Angelina alianza kukumbuka tukio zima.
Mimi nitakusaidia kutoroka ila ninaomba unisaidie kuwakata hawa wafungwa wenzako titi la kushoto. Hapana mimi siwezi, kama masharti ndio hayo bora nibaki humu gerezani. Usiwe mjinga, kuna hii dawa utaiweka kwenye chakula kila mfungwa atakayekula lazima atalala usingizi wa pono. Kumbe!!, alisema Angelina huku akipokea ile dawa. Afande Dickson akaendelea kumpa maagizo kwamba hawa wafungwa wakilala utanisaidia kuwakata titi la kushoto. Angelina akauliza hivi
"Kwanini unahitaji matiti?"
"Na unayapeleka wapi hayo matiti?."
Afande Dickson alicheka sana kisha akasema ipo siku utajua, ila kwa leo ninaomba unisaidie kazi yangu. Nami nitakutorosha hapa gerezani. Baada ya Angelina kumaliza kusimulia. Yule Afande mrefu anayejulikana kwa jina la George alitikisa kichwa kisha akasema kumbe ndio maana, kisha akakumbuka kwamba wakati anaripoti kazini aligongana na Afande Dickson. Baada ya kugongana begi la Afande Dickson lilimponyoka na kudondoka chini. Ghafla lile begi likafunguka lakini Afande Dickson aliwahi kulifunga kisha akaondoka kwa kasi sana. Afande George alimtizama kisha akamuuliza kwamba uko sawa kweli. Ndio. Niko sawa, kisha akaingia ndani ya gari lake na kuondoka kwa kasi sana. Wakati Afande George anatupa macho pale begi lilipokuwa limedondoka akakutana na michirizi ya damu.
****
Mbona huyu anayeuza amefanana na mimi, wakati Kelvin akiendelea kujiuliza alisogea mpaka dukani kwake. Kabla Kelvin hajasema neno, alisikika mteja mmoja akisema kumbe ninyi ni mapacha. Kelvin alisema huyu si ndugu yangu. Wewe ni nani?. Na ni nani kakupatia ruksa ya kuuza katika duka langu. Yule kijana alikuwa amenyamaza kimya. Si ninakuuliza wewe, usijifanye unisikii alisema Kelvin huku akiwa amenyanyua magongo yake ili ampige.
Ghafla alifika Deborah, nakusema na bado ulifikiri ukinipa talaka ndo umetatua tatizo badala yake umeishia kuwa kilema. hahaaa!!, unajipya Kelvin kwanza ninajuta kukufahamu. Achana na mimi, hebu toka hapa. Chuma ulete wewe, unafikiri unanimudu hata kama nikiwa mlemavu shida yako nini. Kwani ninapumua kwa kutumia pua zako. Utajua mwenyewe alisema yule Deborah na kuondoka.
Mama mdogo alinisihi nisifanye chochote pale dukani kwangu lakini nilimwambia mama mimi simjui huyu mtu anayeuza katika duka langu. Mama mdogo alininong'oneza kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akaita bajaji tukaondoka pale. Baada ya nusu saa tulifika nyumbani Tandika. Mama mdogo alinisihi nisiwe na wasiwasi kisha alichukua simu yake na kumpigia mtaalamu Nungunungu. Baada ya mtaalamu kupokea mama mdogo aliweka "loud speaker", kisha maongezi yakaanza.
Haloo, mtaalamu.
Ndio, ninakusikiliza.
Hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui hatima ya mwanangu, kabla mama mdogo hajaendelea kuzungumza. Ghafla mtaalamu alimkatisha na kumwambia hiyo ni sehemu ya kazi ya mfupa wa simba kwa hiyo msiwe na hofu. Yule aliyedukani ni huyohuyo Kelvin ile si ajali bali ni kiini macho au mazingaombwe ya mfupa wa simba. Lengo la ile ajali ni kumfanya Kelvin awe tajiri zaidi.
ITAENDELEA.....
Je, Afande George atachukua hatua gani baada ya kuona michirizi ya damu. Upande wa Pili Kelvin anaambiwa asiwe hofu atakuwa tajiri mkubwa. Na ile ajali ilikuwa ni mazingaombwe. Ili kujua nini kitaendelea usikose kusoma sehemu ya 7 ya hadithi yako nzuri ya THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI).
0 Comments