Sasa mtaalamu vipi kuhusu mwili wangu, mimi sasa hivi ni mlemavu. Mtaalamu Nungunungu alicheka sana baada ya kusikia vile kisha akasema ondoa hofu. Wewe si mlemavu amini ninachokwambia, ila kuna kitu nahitaji ukifanye. Ukishafanya hicho kitu hiyo hali itatoweka kabisa. Kitu gani?,aliuliza Kelvin huku akijitazama mwili wake.
Mtaalamu Nungunungu akasema inatakiwa usiku unapolala uendelee kuukumbatia mfupa wa simba na utalala nao kwa muda wa siku tano tu. Sawa mtaalamu, kwa hiyo nikifanya hivyo tu hii hali inatoweka. Ndio, alisema mtaalamu. Mama mdogo akasema asante. Mtaalamu akasema karibuni tena. Mama mdogo alikataa simu huku akinambia kuwa kijana wangu ondoa hofu baada ya siku tano utakuwa Kelvin wa ukweli. Mmmh haya ngoja nisubiri.
Ulipofika usiku Kelvin alifanya kama alivyoagizwa na mtaalamu, aliukumbatia ule mfupa katika kifua chake kisha akapitiwa na usingizi. Ilipofika saa tisa usiku alishtuka na kukuta funza wamejaa katika kitanda chake. Pembeni kulikuwa na simba mkubwa akiunguruma. Simba yule aliendelea kuunguruma huku akitembea kuelekea kwenye kitanda cha Kelvin. Kelvin alisema ;
"Mungu wangu!!!! "
"Leo ndio mwisho wa kuishi"
Aliongezea kwa kusema lazima nitaliwa na huyu simba alisema Kelvin huku akitetemeka kwa woga. Muda huohuo wale funza walikuwa wamejaa pale kitandani
Yule simba alisogea mpaka kwenye kitanda cha Kelvin kisha akatoa ulimi nje. Ule ulimi wa simba ulikuwa na damu nyingi sana. Kelvin alizidi kuogopa zaidi, alipiga kelele lakini sauti haikusikika. Leo ni siku yangu ya kufa alijisemea huku akifumba macho na kulala kifudifudi huku akisali sala ya mwisho. Ghafla alipitiwa na usingizi mzito. Alipoamka asubuhi hakuamini kile alichokiona.
****
Wakati Afande George anatupa macho pale begi lilipokuwa limedondoka akakutana na michirizi ya damu, lakini alipuuzia tu, wala hakuhisi kitu kibaya. Haya yote Afande George alikuwa anawasimulia askari wenzake. Kwa hiyo lile begi limebeba matiti ya hawa wafungwa aliuliza askari aliyekuwa amevaa kiraia. Ndio, lazima itakuwa hivyo, alijibu Inspector George. Angelina alikuwa akilalamika tafadhali mnisamehe mimi nilishnikizwa tu, bila shinikizo la Afande Dickson nisigeliwakata wafungwa wenzangu titi la kushoto. Yule askari aliyevaa kiraia alimkaripia Angelina.
"Wewe mpumbavu"
"Wewe Muuaji katili kaa kimya"
Aliongezea kwa kusema funga bakuli lako hilo. Inspector George aliuliza huyu Afande Dickson atakuwa anapeleka wapi matiti ya wafungwa. Hata sijui alijibu yule askari aliyevaa nguo za kiraia. Bila kupoteza muda Inspector George alijaribu kumpigia simu Afande Dickson. Simu iliita bila kupokelewa. Alijaribu tena kupiga lakini bado simu haikupokelewa. Huyu Afande Dickson kashatushtikia. Hebu njooni ofisini tuongee alisema Inspector George huku akiondoka chumba cha mateso.
Mkuu wa magereza Pierre John alikuwa ameinamisha kichwa chake katika meza. Alishtushwa na ujio wa askari uliokuwa unaongozwa na Inspector George. Mkuu wa magereza aliwakaribisha huku akiwambia kwamba bado natafakari hii aibu nitaiepuka vipi?. Inspector George aliuliza hivi
Aibu!!!!
Aibu ipi?
Mkuu wa magereza akasema waandishi wa habari wameenda kwenye hospitali waliopelekwa wafungwa na wamepiga picha na kuwahoji wafungwa, kwa kifupi kila kitu kiko hadharani. Tizama hili gazeti la "Sunday news".
Mkuu wa magereza Baada ya kusikia aliyefanya hilo tukio ni Afande Dickson. Mkuu wa magereza hukuamini macho yake alijikuta akinyanyuka katika kiti chake hivi unasema kweli au unamsingizia rafiki yangu Afande Dickson, alisema yale maneno huku akiwa amemkaba Inspector George. Inspector George aling'ata meno yake kisha akasema hiyo inaitwa ;
"Ngumu kumeza"
"Ngumu kutema"
Haijalishi umekunywa na maji. Rafiki yako Afande Dickson ndiye muhusika mkuu akishirikiana na Angelina. Muda huohuo mkuu wa magereza alipiga simu lakini simu ilikuwa haipatikani.
Mkuu wa magereza alisema inamaana Afande Dickson ni mshirikina. Itakuwa hivyo, walisema wale askari. Sawa, hakikisheni mnafunga mipaka yote ya nchi hii ya Israel pia hakikisheni hata unyayo wa Afande Dickson hautoki katika hii ardhi ya Israel. Mkuu wa magereza aliongea kwa hasira kali mpaka macho yake yalikuwa mekundu kama mtu aliyetoka kuvuta bangi.
ITAENDELEA
Je, Kelvin alipoamka asubuhi aliona kitu gani?. Upande wa pili mkuu wa magereza ametoa amri kwamba Afande Dickson atafutwe kila kona ya nchi ya Israel, Je askari watafanikiwa kumkamata Afande Dickson. Ili kujua yote yatakayojili usikose kusoma sehemu ya 08 ya hadithi yako nzuri ya THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI).
0 Comments