THE TRAP (MTEGO )- EPISODE 03

 

Kesho yake asubuhi walifika, tena katika  lile gereza, lakini hali ilikuwa ileile kama ya jana. 

Mjomba wa wale mapacha alimnong'oneza Mwanasheria jambo, kisha wakaondoka pale gerezani, hawakutaka kubishana na wale mapacha tena. Hata askari magereza alishangaa sana, maana alijua watajibizana tena kama ilivyokuwa siku iliyopita lakini haikuwa hivyo. 


"Mnataka kula chakula gani?, aliuliza Bw Christopher paul". Sauti nyororo ikajibu ugali nyamachoma pia tungepata na bia ya Safari Lager ingependeza zaidi. Sawa alijibu, Bw Christopher, kisha akamuita waitress (muhudumu wa kike).


Sauti ya muhudumu wa kike ilisikika: "Habari zenu jamani?. Sijui niwahudumie nini?. Kisha alijibiwa :" Leta ugali na nyamachoma halafu utaongezea na bia ya Safari Lager, bia ya moto au ya baridi. Kabla hajageuka sauti nyingine ilisikika : Wewe Leta za baridi ndio tamu. Yalikuwa majibizano kati ya Christopher na muhudumu kutoka hoteli ya Regency.


Baada ya kula na kunywa, Bw Christopher alimshukuru sana mzee mmoja aliyekuwa amevaa nguo za kimasai, kisha katupia miwani ya rangi nyeusi katika macho yake. 

Bw Christopher alitoa bahasha iliyo tuna, kisha akamuita yule mzee "Chief Zumo hii ni zawadi yako maana umefanya kazi nzuri sana". Chief Zumo alipokea na kusema:"Usijali ni wajibu wangu kuwasaidia. Chief Zumo aliaga, lakini kabla ya kuondoka, alikunywa funda moja la bia, kisha akasema:" Nilitaka kusahau mnajua yule albino amefanyiwa vipimo vingi kule katika hospitali ya Mwananyamara ila imebainika ana.. anaaaa!!... Chief Zumo alisita kusema mpaka vijana wa Bw Christopher wakapata hofu.


Sio tu vijana wa Christopher, hata Christopher mwenyewe alijikuta akiropoka : vipi amekutwa na ngoma nini?. "Hapana ni mjamzito," alisema Chief Zumo. Wakashtuka na kutazamana kisha wakatamka "mjamzitooo?". Ndio yule binti ana mimba. Ghafla simu iliita "samahani kidogo alisema Christopher na kuelekea pembeni kidogo.


Baada ya sekunde kadhaa alipokea na kuitikia haloo?. Upande wa pili alijibu: "Ndio mkuu nakusikia, naombeni mfike kwangu haraka sana". Boss kuna usalama kweli?. Christopher nimesema njooni kwangu haraka sana, kama mtachelewa kufika kwangu mtaujua upande wangu wa pili.


****

Niambie... niambie, niambie Dr. mgonjwa wangu ameshapata fahamu au amekufa. Mzee hebu tulia, mbona una haraka sana, kabla ya yote nataka kujua huyu mwanamke ni nani yako?. Dr. hebu acha siasa naomba unambie kama yuko hai au laa!!. Yuko hai, oooh!! asante Mungu. Kwa kuwa umenambia kwamba huyo mgonjwa wangu yuko hai nitakueleza kila kitu.


Baada ya Dr. Joseph Manoti kuambiwa kila kitu alishusha pumzi, kisha akasema kazi ipo. Unamaanisha nini kusema hivyo. Kabla Dr. Joseph Manoti hajasema akatokea muuguzi Recho akisema Dr, njoo haraka yule mgonjwa ana hali mbaya sana,muda huohuo Dr Joseph Manoti aliondoka. Eti nini?, alisema Mzee Yakobo Kizito, huku naye akinyanyuka kwenye kiti.


Dr Joseph Manoti, alikuta mgonjwa anapumua kwa shida sana. Mhhh, imekuwaje mpaka akawa hivi?,aliuliza Dr Joseph Manoti. Muuguzi Recho alisema huyu mgonjwa alianza kukohoa damu, Sasa sijui tatizo nini?. Dr Joseph Manoti alipima tena mapigo ya moyo, kisha akamwandikia vipimo kama ifuatavyo, inatakiwa achukuliwe picha ya kifua kwa kutumia x-ray machine, ili kubaini chanzo cha tatizo.


Baada siku kadhaa majibu yalitoka, Dr Joseph Manoti alishtuka alipoona yale majibu, alijikuta akisema Mungu amtetee huyu mwanamke.


Itaendelea siku ya kesho jioni. 

Mapacha bado wanaendelea kushikilia msimamo wao, hawataki Kabisa kumpa ushirikiano Mjomba wao pamoja na yule mwanasheria. Lakini upande mwingine Christopher anapigiwa simu na Boss wake kisha Boss wake anamwambia afike mapema nyumbani. Christopher anauliza kama kuna usalama. Boss anamfokea Christopher kisha anamwambia asipofika mapema ataujua upande wake wa pili. Lakini pia Dr Joseph Manoti amepokea majibu gani ya yule mama aliyeokotwa baharini mpaka kufikia kusema Mungu amtetee huyu mwanamke aliyeokotwa baharini. Ili kuyajua yatakayojili usikose kusoma sehemu ya 4, ya hadithi yako nzuri ya THE TRAP (MTEGO).  

Post a Comment

0 Comments