Ama kweli ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni. Ni ngumu kuamini lakini ukweli ndo huu hapa.
Karibu katika simulizi hii ya kusisimua kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Ilikuwa siku ya jumatano huko wilayani kakonko mkoani kigoma, ndipo Sarah mke wa Braison aliyekaa kwenye ndoa kwa takribani miaka 3 hivi bila kuona dalili yoyote ya kupata mtoto alipomwambia mmewe,
“Mme wangu…” alimwambia kwa tabasamu.
“Naam…”
“Nina habari njema…”
“Zipi hizo mke wangu ?”
“Nikwambie au nisikwambie?” Alimshika kwenye bega.
“‘Sasa kwanini usiniambie..?” Alimuuliza.
“‘Ayaa ngoja niseme,!. Najihisi kuwa mjamzito…”
“Hee! acha utani ..! ” aliongea kwa mshutuko.
“‘Kweli kabisa mme wangu…”
“Umejuaje?”..
“Yaani sijaona mwezi wangu kabisa afu najisikia mwenye kichefuchefu..”
“Mhh..mwezi ndo kitu gani?” Alimuuliza
“Jamani kwani hujui, yaani sijaona siku zangu..”
“Hee!, sipati picha kama nami naweza kupata mtoto na wewe. Kikubwa iwe siri yetu na kesho asubuhi na mapema twende hospitali”
“Sawa mme wangu yaani ninafuraha kweli…”
“Hahah ebu punguza furaha tukapime kwanza”
Kesho yake asubuhi na mapema, waliongozana kuelekea hospitali huku wakijihisi wenye aibu mara baada ya kuongozana bila mtoto.
Braison baada ya kukaribia hospitali, alisimama kisha akageuza shingo nakumwambia mkewe,
“‘Mke wangu, nakupeda sana tena sana lakini nakuomba nibaki hapa nikusubiri maana sijisikii kwenda hospitalini hapo..”
“Mhh kwanini ?!, “
“Naona aibu mke wangu kuona hata vijana walioa juzi tayari wana watoto..”
“Mme wangu usijali kuhusu hilo na mtoto ni mpango wa Mungu. Nina imani na matumaini makubwa tutapata mtoto..”
“Nenda kwanza nakusubiri hapa…”
Baada ya kauli hiyo, Sarah akiwa amekunja uso alielekea hospitali.
Aliketi kwenye benchi ndipo aliposikia tangazo kutoka kwa nesi kuwa,
” Wote mliokuja kupima ujauzito kwa mara ya kwanza , mnatakiwa kuja na wenzi wenu”.
Sarah bila kuchelewa, alinyanyuka na kumfuata Braison.
“Wanakuhitaji…” alimwambia.
“Hee! Wananihitaji ili nifanye nini sasa!. “
“‘Bwana ndo utaratibu uliopo sasa hivi…”
“‘Kwahiyo namimi wananipima ujauzito au?”
“‘Bwana we twende kwani unaogopa nini?. Kuna wanaume wenzio wengi nimewaona..”
“Ni vizuri kujua wanataka kunifanya nini maana..” alikatisha maneno kisha Sarah akamvuta na kuongozana naye.
Braison alikuwa anatembea kwa kutetemeka kwelikweli huku akiwa kama anataka kutimua mbio.
Alijikaza mdogomdogo na hatimaye wakafika hospitalini hapo kisha Sarah akaingia chumba (Nesi).
Kabla hajamsikiliza, alimuuliza.
“Umekuja na mwenza wako?”
“Ndiyo…”
“Ebu kamuite aingie ndani..”
Sarah alimfata Braison kisha akamwambia kwa sauti ya chini.
Braison alijikuta mwili mzima unatetemeka lakini alikubali kwenda.
“‘Karibu…” Nesi aliwakaribisha.
“‘Asante…” Braison aliitikia.
“Samahani kwa usumbufu lakini ndivo mwongozo unavyotaka kila mama anayetaka kupima ujauzito kuja na mwenza wake…”
“‘Sawasawa. “
“Sasa kabla ya kuendelea, tutapima afya zetu hasa kuona kama tupo salama juu ya VVU au la”
“‘Hee! Yamekuwa hayo tena!, kama ni hivyo basi..basi…”Braison alifoka.
“‘Kuwa muelewa, kupima afya yako inasaidia kuishi kwa matumaini na kujikinga zaidi. Kikinge inamsaidia mtoto mtarajiwa kuweza kuwa salama” Nesi alimwambia Braison.
Baada ya kuambiwa hivo, Braison alitulia kidogo huku akikimbuka ni miezi mitatu imepita tangu binti wa kinyarwanda aliyetembea naye (Guest house), afariki .
Mapigo ya moyo yalipanda na kushuka kwa Braison hali iliyomuogopesha sana Sarah.
Nesi aliwapeleka kwenye chumba cha maabara ambapo walitolewa damu kwa ajili ya vipimo.
“‘Subirini kidogo kama dakika 5 nawapa majibu” aliwambia.
Bila kupoteza hata dakika 1, Nesi alimuita Braison aje peke yake ili ampe majibu.
“Braison….”
“Naam…”
“Nakuomba…”
Kwa hofu kubwa alienda kupokea majibu.
“Relax, jisikie huru…” alimwambia….
0 Comments