Vilio vya watoto wawili, vilisikika katika Gereza la Upanga, Jijini Dar es salaam, hakuna aliyejua nini kilichopelekea watoto mapacha (Joel na Jose) kuwekwa mahabusu, lakini kwa mbali ilisikika sauti ya msimamizi wa watoto gerezani 'patron' ikisema :"Naombeni msilie, futeni machozi, yote yatakwisha".
Wakati Patroni anataka kusema neno jingine, alishtushwa na sauti nzito ya kiume, ikiuliza? "Wapwa zangu ni kweli mmebakaa?". Ukimya ulitawala kwa sekunde kadhaa, ghafla Joel akasema :huyu Jose ndie kasababisha mpaka huu msala umetukuta.
Sauti ile nzito ilisikika tena ikiuliza : "Ulifanya nini Jose?". Ilikuwa ni sauti ya mjomba wao ikidadisi ili kujua kisa cha watoto hao kutumbukia gerezani, lakini kabla mtoto hajajibu Patroni ilibidi aingilie kati na kusema. "Mimi niliangalia taarifa ya habari ndio nikajua kwamba hawa wapwa zako wako mahabusu kwa kosa la ubakaji. Ila ukweli wote wanaujua wao.
Mjomba mimi nitasema ukweli, unajua msema kweli ni kipenzi cha Mungu, iko hivi; "tulikuibia pesa tukapanda Gari na kwenda msitu wa Magoroto". Msitu wa Magoroto? huu msitu si upo Tanga, wilaya ya Muheza?, alihoji mjomba na Jose akasema Ndio.
Mjomba aliendelea kuhoji "mlienda huko kufanya nini, nyie watoto? si juzi tu ndio mmeanza likizo?, kwa nini hamtulii nyumbani, alisema mjomba kwa sauti ya ukali. Joel aliendelea kulia huku akimnyoshea kidole mwenzake na kusema: "Huyu Jose ndio amesababisha, ndiye aliyenishawishi".
Patroni alimuuliza Joel kwa sauti ya upole huko Magoroto mlienda kufanya nini?. Joel alimtazama Jose kisha akasema : "Kaka yangu Jose alinambia eti msitu wa Magoroto ni mzuri sana, twende tukaone jinsi Mungu alivyoupendelea. Tulipofika kwenye msitu huo, tukiwa bado tunashangaa, tukasikia sauti ya mwanamke akipiga kelele, ikatulazimu tusogee ili tujue kuna tatizo gani?. Baada ya kusogea hatukuamini kile tulichokiona.
****
Mzee Yakobo Kizito, alikuwa anaweka nyavu zake katika bahari ya Hindi, alishangaa kuona mwili wa mtu unaelea katika bahari hiyo. Ilimlazimu kuacha nyavu zake, akaanza kuogelea alipoukaribia ule mwili aliona pembeni yake kuna mamba mkubwa anakuja. Mzee Yakobo Kizito aliogelea kwa kasi zaidi, lakini mamba naye alikuja kwa kasi zaidi. Hapa nisipotumia akili huyu mamba atakula huu mwili, alisema Mzee Yakobo Kizito. Mara ghafla damu zilitapakaa katika ile bahari.
Itaendeleaa....
Usikose kusoma sehemu ya pili ili kuijua hatima ya mapacha (Joel na Jose). Upande wa pili pia Usikose kufuatilia ili ujue je ule mwili uliokuwa unaelea katika bahari uliliwa na mamba au je Mzee Yakobo Kizito alifanya kitu ili kuokoa ule mwili uliokuwa unaelea.
0 Comments